Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

vichekesho na vimbwanga vya mitandaoni

*Madem mna roho MBAYA kweli* *Unakutana na dem mgahawani* *Una mpa ofa ya* *supu ya mbuzi* *Baadae una mpa* *hela ya taxi* *Cha ajabu ukimpa namba ya simu* *Anakusave* *SUPU YA MBUZI* 😢😢😢 *HIVI KWANINI* ............................................................ 🤔🤔 *Wakati mzungu katengeneza simu, na unaitumia kwa mawasiliano ya video(video call/snap video) kisha unaita teknolojia...🙆‍♂🙆‍♂Chakushangaza bibi yako akitumia kioo kukuangalia unapokua mbali eti waita uchawi...🤣😂🤣😂🤣😂hivi waafrika tuna laana gani??🙆‍♂🙆‍♂🙆‍♂* ............................................................ *Wife :Baby leo nimeona iphone8 kwenye duka la simu mjini, ni nzuri😍 *Husband : Vipi umeipenda🤔 *Wife: Nimeipenda sana mpenzi wangu😍😍😜&#128540...

Vichekesho na vituko vya mitandaoni

Picha
Vichekesho na vituko mitandaoni *Hongeren wadada woote ambao mnajitahid kumechisha rangi ya nguo na mikoba yenu kuliko watoto na sura za baba zao* 😀😀😀😀😀😀 .......................................................... *HARMONIZE NI MSANII ANAETOKEA KATIKA KABILA LA WAMAKONDE ANAJIITA "KONDE BOY" SASA NAPATA SHIDA KUJUA KAMA ANGETOKEA KATIKA KABILA LA WASUKUMA ANGEJIITA VIPI?*🙌😹😹😹😹 .......................................................... *Jana nmeota nmenunua gari sa wakat naendesha Si likakwama njian nikashuka nikaanza kulisukuma ile kuamka Si nkajikuta nipo na kitanda jikon😡😡😡😡😡* .......................................................... *Hakuna siku mbaya kama siku unayopita nje ya kanisa halafu unamsikia mchungaji anasema, "amini nawaambieni nje kuna shetani anapita...

jinsi ya kumiliki biashara yako

Watu wengi wamekua wamitamani kumiliki biashara au kuwa wajasiriamali lakini hawajui ni njia gani wafuate  leo nimekuandalia haya kwa uchache ufikie ndoto zako Usiruhusu orodha hii kukuogopesha. Hatua ya kwanza ya kuwa na mafanikio ni kuelewa ujuzi gani unao na ambao unakosa. Stadi hizi zote unaweza kujifunza, kwa hivyo ukitambua unakosa kitu fulani,usisite kujifunza. Linapokuja suala la mauzo, masoko na fedha unaweza kuchukua kozi, kujifunza mwenyewe au kujifunza kutoka kwa watu walio karibu nawe. ukishafahamu utakuwa tayari kuzindua biashara yako. 1. Uwezo wa kusimamia fedha Ili kuendesha biashara kwa ufanisi. unahitaji kuwa na uwezo wa kusimamia fedha. Jibu maswali haya kuhusu fedha zako binafsi kwanza: Unajua wapi fedha zako huenda kila mwezi? Je, unazalisha zaidi ya unayotumia? Ikiwa jibu sio kwa yote mawili, utajitahidi kusimamia pesa yako na biashara pia. Anza kwa kupata fedha zako binafsi, utumie kwa utaratibu kwa kuzingatia bajeti ya biashara. 2. Uwezo wa kuzalisha. H...

MIMEA YA KALE CHANZO CHA UDONGO

Nakumbuka siku moja nikiwa nyumbani napiga stori na mdogo wangu sijui aliwaza nini akaniuliza swali "hivi kaka udongo unatokana na nini?" Nilimjibibu "udongo unatokana na kuvunjika kwa miamba na kuwa vipande vidogo sana ambavyo tunaviita udongo" "Kwahiyo kaka unataka kuniambia miamba inapungua ukubwaaa kilasiku" "Ndio" "Kwahiyo kaka milima nayo kilasiku inapungua urefu?" Sikumbuki nilimjibu nini . ila kutokana na swali lake nimekua nikijiuliza hivi udongo unatokana na nini? nikweli unatokana na kuvunjika kwa kwa miamba Pengine unaweza kujibu upepo, mvua na barafu zilisababisha miamba kuvunjika na kubadilika kuwa udongo, lakini hivi karibuni Watafiti wamenijibu swali langu  lakini wameniacha na mshangao nimeamua nikushirikishe na wewe watafiti hao wanasema waligunduwa kuwa mimea ya kale kwenye nchi kavu huenda ndio chanzo muhimu ya udongo na mchanga duniani. Miamba aina ya shale na slate ambayo iliundwa na chembe ndogondogo za...

MITI ILITANGULIA KUISHI NCHI KAVU MIAKA 500

Picha
M ITII ILIANZA KUISHI DUNIANI   MIAKA 500 ILIYOPITA Je umewahi kujiuliza maswali kuwa miti ilitangulia duniani miaaka .mingapi? Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Taasisi ya sayansi wa China unaonesha kuwa mimea ilianza kuishi kwenye nchi kavu katika miaka milioni 500 iliyopita, wakati ambao ni mapema zaidi kuliko uliokadiriwa zamani. Wanasayansi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu lini mimea ya kale ilianza kukua kwenye nchi kavu. Ingawa visukuku vinaweza kutoa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu mabadiliko ya viumbe, lakini ni vigumu kupata visukuku kamili vya kutosha. Watafiti kutoka Bustani ya mimea ya kitropiki ya Xishuangbanna ya taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza wametafiti data za transcriptome kwenye seli za aina 103 za mimea na makumi ya visukuku, ili kuhesabu lini mimea ya kale ilianza kuishi kwenye nchi kavu. Baada ya kuhesabu, watafiti wamesema mimea ya kale ilianza kuishi kwenye nchi kavu katika miaka milioni 500 iliyopita katika kipindi cha Ca...

NJIA ZA KUZUIA KUKOROMA UNAPOLALA

NJIA ZA KUZUIA KUKOROMA UNAPOLALA Watu wengi wana tabia ya kukoroma wanapolala, lakini kukoroma siyo kuzuri sana kwani familia yako pengine ishindwe kupata usingizi vizuri kutokana na makelele ulnayoyatengeneza na kwa upande mwingine, kukoroma kunamaanisha kuwa pumzi zako haziko sawa, hata baadhi ya wakati kukoroma kunaweza kusababisha kukosa pumzi na kupelekea kifo. Kwa hivyo, Leo nimewaandalia njia nne za kuuzui tatizi hilo nazo ni 1. kuchagua mito laini na inayoweza kufanya shingo yako iwe vizuri, ambayo itasaidia kupumua unapo lala mitindo isiyoeleweka inachangia mtu kukoroma kwani hewa haipiti vizuri 2.  kutumia mashine ya (humidifier) ili hewa ndani ya chumba iwe ya unyevu na kuepuka koo yako kuwa kavu; ila sina uhakika kwa hapa Tanzania yanapatianane na yanaunwaje 3. kunywa asali kidogo kulainisha koo yako na Kufanya koo lako lisiitoe saut unapo pumua. usinywe pombe kwani inapandisha shinikizo lako la damu na kuwa juu na kubana koo lako pamoja na kuzuia pumzi. 4. k...

SAYANSI: Wanasayansi wamevumbua betri ya li-on inayowezakutumika kwenye joto la

Picha
     Wanasayansi wa China wamesanifu betri ya Li-ion inayoweza kutumiwa katika joto la nyuzi 70 sentigredi chini ya sifuri, ambayo inatazamiwa kutumiwa katika maeneo yenye baridi kali duniani na hata anga ya juu.      Kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Fudan kinachoongozwa na Xia Yongyao kimetumia kemikali aina ya Ethyl Acetate inayoweza kupitisha umeme katika mazingira yenye baridi kali kuwa elektrolaiti, na kutumia kemikali za kikaboni za PTPAn na PNTCDA kuwa elektrodi mbili.       Elektrolaiti ni kemikali inayozifanya ioni zitiririke kati ya elektrodi mbili za betri, lakini mabadiliko ya kikemikali kati ya elektrolaiti na elektrodi hayawezi kudumu katika mazingira yenye baridi kali.       Uwezo wa betri ya zamani ya Li-ion katika joto la nyuzi 20 sentigredi chini ya sifuri unapungua na kuwa nusu tu, na uwezo huo umepungua hadi kuwa asilimia 12 tu ya hali ya kawaida katika joto la nyuzi 4...

AFYA:KUCHEZA DANSI KUNAPUNGUZA KUZEEKA KWA UBONGO

Utafiti mpya umeonesha kuwa ikilinganishwa na mazoezi rahisi ikiwemo kutembea, kucheza dansi kunaweza kupunguza zaidi uzeekaji wa ubongo. Utafiti wa awali umeonesha kuwa mazoezi yanaweza kuusaidia ubongo kupambana na uzeekaji, lakini haukuonesha mazoezi ya aina gani ni mazuri zaidi. Utafiti huo mpya umelinganisha mazoezi ya aina mbili tofauti yaani kucheza dansi na mazoezi ya uvumilivu. Matokeo yameonesha kuwa kucheza dansi ni nzuri zaidi. Watafiti wa Ujerumani wamewashirikisha wazee waliojitolea wenye umri wa wastani wa miaka 68. Katika utafiti wa miezi 18, wazee hao wote wamejifunza kucheza dansi au kufanya mazoezi ya uvumilivu kila wiki. Kikundi cha mazoezi ya uvumilivu kinatakiwa kurudia kufanya mazoezi ambayo ni pamoja na kupanda baiskeli na kutembea. Kikundi cha kucheza dansi kinatakiwa kujifunza mtindo mpya wa dansi kila wiki. Kutokana na uangalizi wa eneo la Hippocampus la ubongo, mazoezi hayo mawili yote yanaweza kuinua uwezo wa eneo hilo, lakini kucheza dansi kunaweza kui...

Ujumbe mkongwe zaidi uliohifadhiwa kwenye chupa

Picha
Familia moja nchini Australia umepata ujumbe ambao ni mkongwe zaidi uliokuwa umehifadhiwa katika chupa, Ni takribani miaka 132 tangu ujumbe uliokuepo kwenye chupa urushwe katika bahari. Chupa hiyo yenye ujumbe iliokotwa na bwana Tonya Illman wakati akiwa anafanya matembezi katika ufukwe wa bahari huko pembezoni,magharibi mwa Australia. Wakati ameokota chupa hiyo ,Tonya hakujua ni nini kilichoandikwa mpaka alipofika nyumbani kwake na kuioka karatasi hiyo katika jiko la kuokea(Oven). Wataalamu wamethibitisha kuwa ujumbe huo ni wakweli na ulitupwa kutoka meli moja ya Ujerumani. Ujumbe huo uliokuwa umeandikwa tarehe 12.6.1886, na ilikuwa sehemu ya jaribio ambalo lilifanywa na meli hiyo ya ujerumani ili kubaini njia ambayo meli za taifa hilo zilikuwa zinapita baharini. Miaka iliyopita kumbukumbu za "Guiness world "zilisema ujumbe ambao uliowahi kutupwa kwa kuhifadhiwa kwenye chupa na kupatikana ulikaa miaka 108. Hata hivyo mtu huyo alipoliokota ujumbe huo alidhani labda hiy...

Jinsi ya mwanamke kujikomboa na dimbwi la umasikini: jifunze nami

Picha
Ikiwa leo ni siku ya wanawake duniani leo nimewaandalia makala fupi itakayo kuondoa katika janga la umasikini na kuaacha kuaendelea kuwa ombaomba kwa mwanaume/mpenzi wako Kama wewe ni mmojawapo wa wanawake wanaohitaji kutengeneza utajiri mkubwa wa kudumu na kuishi maisha yenye uhuru wa kifedha katika maisha yao yote ni vizuri usome hapa. Ila kama wewe ni miongoni mwa wanawake walio tayari kuendelea kuishi maisha ya umasikini pasipo na nia ya dhati ya kuondokana nao, ni vyema nikushauri usisome hapa kwa sababu unaweza kubadilika moja kwa moja na maisha yako yakawa tofauti na namna unavyotaka. Niliwahi kusema, “Kuwa tajiri si dhambi bali kuwa masikini ni kuchagua.” Hivyo basi uchaguzi ni wako kuendelea kuishi katika hali ya umasikini kwa hofu ya kuamua kuchagua kuwa miongoni mwa matajiri, au kuchagua utajiri kama sehemu pekee ya kukupa nafasi ya kuwa huru kiuchumi. Robert Kiyosaki mwalimu na mtaalamu wa masuala ya fedha na uwekezaji nchini Marekani aliwahi kuandika...

Wanawake huathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi

Picha
Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi zaidi ya wanaume. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake. Majukumu yao kama walezi na wanao hudumia familia kwa karibu zaidi huwafanya kuwa katika mazingira hatari zaidi wakati wa mafuriko na ukame unapotokea. Makubaliano ya mjini Paris mwaka 2015 yaliweka kipaumbele maalum cha kuwawezesha na kutambua kwamba wanawake huathiriwa kwa kiasi kikubwa zaidi katika jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Afrika ya kati, eneo ambalo ziwa Chad limetoweka kwa asilimia 90, hali inayolazimu wenyeji wa eneo hilo kuhama na kuwa katika mazingira hatari. Kila wakati ziwa linapopungua ,wanawake wanalazimika kutembea kwa muda mrefu kutafuta makazi mapya. Wakati wa kiangazi wanaume wanaenda mjini na kuwaacha wanawake vijijini kuangalia jumuiya. Hivyo wanawake wanalazimikia kufanya kazi zaidi ili kutu...

Jinsi ya kuchagua perfume zuri

Picha
Kuna maelfu ya perfume madukani, lakini sio perfume zote ni nzuri kwa kila mtu, kwa hiyo ni muhimu kuchagua perfume ambayo itamfaa mtumiaji ili kuepuka disappointment. Perfume unapoinusa inagawanyika mara tatu, wenyewe wanaita NOTES, yani kile unachokisikia na ukali wake unavotofautiana. Hiyo ndo sababu perfume zingine ukinunua ukajipuliza zinakuwa kama harufu inabadilika kadri inavosikika inapojichanganya na hewa, zingine hupoteza mvuto kabisa wakati nyingine huendelea kupendeza kadri mda unavoenda.  Hizi notes ziko tatu, Top Note(Harufu unayoisikia mwanzo kabisa) ambayo inapotea haraka, kuna middle note yaani harufu ya kati ambayo utaisikia baada ya harufu ya mwanzo kupotea na mwisho Note ya tatu ambayo huitwa Basic Note yani harufu haswa ya hiyo perfume baada ya harufu za mwanzoni kupita,ambayo ndo itabaki muda mrefu. Inashauriwa unapochagua perfume ya kununua usilipe mpaka umeisikia vizuri mpk mwishoni hata dakika 20 hivi. Perfumes hugawanywa kulingana na aina ya harufu amba...

Jinsi ya kuwa gentlemen wa kisasa

1. Muungwana wa sasa usali na kuamini MUNGU yupo. Kama sote tujuavyo MUNGU ndio kila kitu kwenye maisha yetu ya kila siku kwani tunapewa pumzi bure na pia anatulinda na maadui tunaowafaham na tusiowafahamu.hivo muungwana wa kisasa umuamini MUNGU na uwe na hofu ya MUNGU. 2. Vaa vizuri bila kujali tukio. kama wengi tunavyojua kua uvaaji wako ndo unaonesha wewe ni mtu wa aina gani,hivo vaa vizuri nguo zinazokufiti mwili na zisiwe kubwa au zinazobana kupita kiasi.usivae milegezo. 3. Kutanisha macho kwa macho wakati wa kuzungumza na mtu. Inaonyesha kiwango cha ujasiri, uaminifu na maslahi ya kweli pia uongeza mkazo kwenye kile unachokiongea. 4. Ustaarabu hauna gharama yoyote, lakini ndio kila kitu. Kama neno linavokwenda, tabia nzuri ni hitaji daima katika mtindo, na kila muungwana wa kisasa anapaswa kujua kwamba tabia zinaweza kufungua milango ambayo elimu haiwezi. 5. Lugha mbaya inaonyesha ukosefu wa elimu. Wakati wa kuzungumza angalia sana maneno unayotamka yasiwe yenye kuonesha...

vichekesho: jifunze nami

  Soma hii ! Eti mzee anadai anataka kumsikiliza Nyerere saivi ..! kichekesho: "Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari Angalia kilichompata huyu katika ziara za kushtukiza kichekesho: "Mimi Nimecheka sanaZIARA ZA KUSHTUKIZA Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.\n\nNikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ...

SABABU ZA WANAWAKE KUPIGA KELELE WAKATI WAKIFANYA MAPENZI

Picha
UTAFITI: KWANINI WANAWAKE HUUPIGA KELELE WAKATI WA KIFANYA MAPENZI Mwaka 2011 watafiti wawili mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Lancashire na mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Leeds wote wa nchini Uingereza walichapisha utafiti wao walioufanya uliokuwa ukihusu utoaji wa sauti wa kati wa kujamiina. Walitaka hasa kujua kwanini wanawake hutoa sauti hizo. Katika utafiti huo, waliwahoji wanawake 71 wenye umri kati ya miaka 18 na 48 ambao hushiriki mapenzi mara kwa mara juu ya utoaji wa sauti wakati wa kujamiiana. Katika utafiti huo ulibaini kuwa wanawake wengi huto sauti hizo lakini sio pale tu wanapokuwa wamefika kileleni. Asilimia 66 walisema kuwa hutoa sauti wakati wa kujamiina ili kuwasaidia wenza wao kufika kileleni haraka, wakati asilimia 87 walisema kuwa hutoa sauti hizo ili kuwaongezea wenza wao kujiamini kwa kile wanachokifanya kuwa wapo sawa. Wanawake walieleza kuwa mara nyingi hutoa sauti wakati wenza wao wanapofika kileleni. Baadhi pia walieleza kuwa sauti hizo huwasaidia kuw...

Fuata hatua hizi kupata mpenz ya kweli

FUATA HATUA HIZI KUPATA MAPENZI YA KWELI Niongee kidogo kuhusu sumu ya mahusiano yetu KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi. 1. WIVU WA KUPINDUKIA Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufany...