vichekesho: jifunze nami

 Soma hii! Eti mzee anadai anataka kumsikiliza Nyerere saivi..!

kichekesho: "Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari

Angalia kilichompata huyu katika ziara za kushtukiza

kichekesho: "Mimi Nimecheka sanaZIARA ZA KUSHTUKIZA Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.\n\nNikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza. Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu. Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa. Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, “Salama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka “Samahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani"

Dada azimia kanisani akifunga ndoa

kichekesho: "NDOA inafungwa KANISANI Mchungaji akauliza-Yeyote mwenye Pingamizi La Ndoa hii kufungwa aje Mbele, KIBABU kikasimama na kwenda Mbele,Bibi harusi akaanguka na akazimia ghafla Mchungaji- Tuambie Babu Pingamizi Lako!Babu-Nimeamua kuja mbele,kule nyuma sisikii vizuri! watu hoiiii!!hata mimi

Cheki huyu alivyoumbuka baada ya simu kuita msikitini

kichekesho: 'Jamaa alisahau kuzima simu akiwa msikitini anaswali GHAFLA simu ikaita akaingiza mkono ili aikate, kwa bahat mbaya akaminya cha kupokelea, alipohangaika kuzima akajikuta kaminya laudspika ikasikika sauti ''ETI HONEY UMESEMA NIWEKE KITIMOTO KIASI GANI?

Angalia mvulana fala kuliko wote

kichekesho: "ALITOKEA MVULANA MMOJA:MVULANA: Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?DAKTARI: Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!MVULANA: Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.DAKTARI: Nashukuru umeelewa somo!

Mambo ya Mabinti haya

kichekesho: "Binti: Hallow mpenzi, Mambo Jamaa: Poa babyBinti:Uko wapi? Jamaa: Niko town napata lunch Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini? Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.Binti: Kwanini dear?Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli"

Hawa machizi wamezidi sasa

kichekesho: "Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.Chizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.Chizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbelenda!balaaa"

 Maana ya msemo siri haina wawili hii hapa

kichekesho: SIRI HAINA WAWILI Imesimuliwa kuwa Palitokea mtu maskini jina lake ban hashim na alikuwa na mke maisha yake alijishuhulisha katika kilimo.Siku moja wakati akilima aliokota fungu la dhahabu shambani alilibeba akafurahi na kushukuru licha ya kuwa alikuwa na hofu sana Kwani alifikiri angelihadithia watu wasingemuamini kwa umaskini wake wangedhani huenda ameiba na hakuna ambae angeweza kuinunua dhahabu hio ila wangemtapeli tu naliondoka akiwa ameibeba dhahabu yake katika mfuko akaingia nayo nyumbani kwake na kuificha bila mkewe kujua chochote Alipofikiria kumwambia mkewe juu ya mali alioipata aliogopea kuwa huenda mkewe akawatangazia majirani kisha wakaibiwa na wezi Akafikiria sana mwisho akapata ufumbuzi aliingia chooni akakaa muda kisha akamfata mkewake huku akiwa na uwoga Kisha akamwambia mke wangu ntayokuambia tafadhali iwe siri wala yoyote asijue nae mkewe alimuahidi kuwa angeiitunza siri hio pasi na mtu kujua nakamwambia nilipoingiaa chooni kujisaidia ghafla walitoka ndege wawili kisha wakakimbia kimaajabu mkewe kuskia hivo alistaajabu kwa lililomtokea mumeweSiku ya pili mkewe alikwenda kwa jirani yake wa karibu kisha katika stori mara akamwambia shoga angu lililompata mume wangu nila ajabu jana kaingia chooni baada ya kujisaidia wakatoka ndege watatu kisha wakaruka kimaajabu jirani alishangaa kisha akamwambia usiseme mume wangu alinikataza nisihadithie Ikapita muda jirani nae siku ameketi na watu akawasimulia jamani mnahabari mke wa ban hashim amenisimulia kuwa mumewe aliingia kujisaidia mara wakatoka ndege wanne wakarukaa kimaajabu habari zikazidi kuenea katika mji wao na kila alie hadithia aliongeza ndege mmoja ,3,4,5,6 mpaka ikafika kwa mfalme kuwa kuna mtu kajisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabuJambo hili lilimshangaza sana mfalme akatuma watu wakamkamate huyu mtu na wamlete kwake ili amuone huenda mtu wa ajabu sanaWalitoka watu wakamfata wakamwambia mfalme anakuita akashuhudie kwako juu ya habari kuwa wewe umejisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabuBasi Alitoka akaongozana na hao watu huku akiwa amebeba mfuko wake wa dhahabu bila ya watu kujua alichobeba mpaka wakafika mbele ya mfalme Mfalme akamwambia je ni kweli wewe ndie ulie jisaidia ndege 100 kisha wakaruka kimaajabu? Ban hashim alicheka kisha akamwambia mfalme hizi habari nilimsimulia mke wangu kuwa nilijisaidia ndege wawili nashangaa zimeenea na kila alieambiwa alipomhadithia mwenzake aliongeza ndege mmoja mpaka imefika kwako niliambiwa kuwa nimejisaidia ndege 99 kisha na wewe ukaongeza mmoja wakatimia 100Mfalme kusikia hivo alicheka kusikia kisa hichi kisha ban hashim akamwambia mfalme mimi niliokota dhahabu shambani nikaona hakuna ataeweza kuinunua sana watanidhulumu au kuniua na kwako sikuweza kukuletea kwani hawaingii ovyoo watu kwa mfalme ndio nikafanya hivi ili niweze kuja kwako kwa urahisi na dhahabu ni hii akaiweka mbele ya mfalme kisha mfalme alimpa pesa nzuri zilizokuwa sawaa na mali yake akarudi na kuishi kwa furaha na mke wake.Kisa hichi kinafunza kuwa ukiletewa habari✉ na mtu basi ichunguze na usizidishe kitu kwani watu huongeza yao au kupunguza kwa kila wanalolisikia na inatufunza mke kuwa na siri na mumewe na sio kuzitangaza kwa majirani Kwani habari zinaruka kama mfano wa vumbi kuenea kwa haraka.Licha ya kuwa ban hashim alipata urahisi wa kuuza dhahabu yake lakini na kama ingekuwa madhara basi angeangamia kwa mdomo wa mkewake Mwisho kisa hiki hakikutaja majina ya wahusika kilipo mfikia ban h

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

HAYA NDIO MAKUNDI 16 YA WATU NA TABIA ZAO

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA