vichekesho na vimbwanga vya mitandaoni
*Madem mna roho MBAYA kweli*
*Unakutana na dem mgahawani*
*Una mpa ofa ya* *supu ya mbuzi*
*Baadae una mpa* *hela ya taxi*
*Cha ajabu ukimpa namba ya simu*
*Anakusave*
*SUPU YA MBUZI*
😢😢😢
*HIVI KWANINI*
............................................................
🤔🤔
*Wakati mzungu katengeneza simu, na unaitumia kwa mawasiliano ya video(video call/snap video) kisha unaita teknolojia...🙆♂🙆♂Chakushangaza bibi yako akitumia kioo kukuangalia unapokua mbali eti waita uchawi...🤣😂🤣😂🤣😂hivi waafrika tuna laana gani??🙆♂🙆♂🙆♂*
............................................................
*Wife :Baby leo nimeona iphone8 kwenye duka la simu mjini, ni nzuri😍
*Husband : Vipi umeipenda🤔
*Wife: Nimeipenda sana mpenzi wangu😍😍😜😜😜
*Husband: Usijali kesho nitakupa nauli ukaiangalie tena
😜😜😜😂
............................................................
mtoto:mama wale wavurana wa pale juu waliniita mama:wamekwambiaje binti yangu? mtoto:waliniambie nipanda mtini ili niwaangulie maembe 😳😳😳 mama:hee binti yangu wale wavurana wahuni tuu maana wakitaka kukuchungulia chupi yako tuuuu👭 mtoto:mama namimi nilijua tu lengo lao👩🏼⚖👩🏼⚖👩🏼⚖👩🏼⚖👩🏼⚖ mama:ulifanyaje mwananguuu👰👰 mtoto:nilivua chupi kwanza ndo nikapanda kuwaangulia maembee🙈🙈🙈 mama:……❓😳😳😳🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
............................................................
Kukutana kwa Uhuru na Odinga katika kusuluhisha tofauti zao kunanikumbusha enzi za raisi wa zamani wa Urusi Mhe. Presvilodiskyovach Petrovzilizevisky.........Najua hilo jina hujalisoma,umeruka,na mimi siendelei kusimulia mpaka ulisome.
Maana sipendelei wavivu😜😜😜😜
*jamani wazazi tujifunze kutoka kwa kambare maana wazazi mtoto akiota ndevu tuu wanaona ni mkumbwa aanze kujitegemea ila mtoto wa kambare anaota ndevu tokea tumbonii ila wazaz wake wanaendelea kumtunza tyuuuu.*
............................................................
WANAUME NA ENZI ZETU!
Enzi za Mwalimu wanaume tulipewa majina stahiki kama vile
MUME WANGU au BABA WATOTO
Enzi za Mwinyi wanaume tuliitwa MABWANA utasikia mwanamke ana muhadisia mwenzie kapata Bwana.
Enzi za Mkapa wanaume tukaitwa MABUZI
Mwanamke ana msimulia mwenzake nime pata Buzi.
Enzi za Kikwete tukapewa majina mazuri na matamu hata ukisikia unafurahi moyoni,
#Baby, Darling,sweety,Honey na mengine mengi.
Enzi hii ya Magufuli sasa!
Pesa hazionekani wanaume tume vurugwa maisha magumu
Wanatuita WAHENGA
Wanawake wa Bongo Mungu anawaonaaaa.
Wanaume kwa Vile Pesa Ngumu,tuna kauli yetu tunakwambia
Mwanaume MASHINE
Dadeki mta elewaa tuuuh!
*Watu Bwana* 😂😂😂
*Utotoni nilikuwa naambiwa simama dede umuone mchumba wako, leo natembea kabisa lkn simuoni* 😒😒😒
............................................................
MOYO WA MWANAMKE NI HATARE
Moyo waliopewa WANAWAKE akipewa Mwanaume hata kwa Siku 2 tu LAZIMA AFARIKI!
Ule uwezo wa kuvumilia Maumivu ya Kuzaa ndio huwa unawafanya wavumilie mambo wanayotendewa na Wanaume kiasi ambacho hadi wewe Mwanaume unajiuliza,
HADI HILI AMENISAMEHE, INAWEZEKANAJE!
Kama kuna jambo Wanaume huwa wanakosea basi ni kudhani kwamba Wanawake ni Wajinga.
Hawajawahi kuwa Wajinga ila Wameumbwa na Moyo wa Uvumilivu uliopitiliza.. Na Mungu aliwatengeneza hivyo makusudi...
Mwanamke anaweza kumvumilia Mwanaume ambaye kwa Miaka 10 hamtimizii mahitaji yake lakini Mwanamke yupo tu..
Uvumilivu ulioje! Mwanamke anayeweza kukaa na Mwanaume mlevi anayempiga ngumi kila akirudi ila yeye yupo tu.. Sio kwamba ni Mjinga,LA HASHA!Ni katika ule Uvumilivu tu.
Kasheshe ni pale Mwanamke huyu ANAPOCHOKA...
Anaweza akavumilia miaka 10...Unampiga...Anakufumania..Humfikishi Kileleni..Ila Siku Akichoka akasema KWAHERI,
Ule Moyo wa Uvumilivu huwa UNAGEUKA na kuwa JIWE GUMU na hata uimbe mashairi ya "Bado ananijia ndotoni ila nikiamka simuoni bado ananijia nikilala Haki ya Mungu sio masihara"
Sijui kaimba nani yule m nimemsahau
Utaimba sana lakini HATARUDI na utabakia kiwete wa mahaba yake daima...
-------------------------------------------------------------------
USHAURI WANGU:
Kabla hajafikia Stage ya KUKUCHOKA, chondechonde kumbuka nayeye ana Moyo,MPE ANACHOSTAHILI!
Usichanganye Uvumilivu wake ukadhani ni Ujinga,ITAKUCOST
*UNAINGIA NA DEMU GETO mara paah!!! KAVUA JEANS NA CHUPI KWA PAMOJA,NDUGU YANGU HAPO TUMIA KONDOMU*😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
............................................................
*Mwanaume unaekojoa ndani kwenye kopo usiku ukiogopa kutoka nje! Ni marufuku kumwambia mpenzi wako kuwa upo tayari kufa kwa ajili yake*....🤚🏽 😂😂😂😂😂
*WATOTO WA SIKU HIZI HAWAJUI KABISA ENZI ZETU UNAWEZA KUCHAPWA KWA SABABU ZIFUATAZO;*
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama, utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa
14. Ukikataa kula, utachapwa
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa
17. Kujitia kisirani, utachapwa
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa...N.K.
*Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni ”HATARI”*
Maoni
Chapisha Maoni