MIMEA YA KALE CHANZO CHA UDONGO
Nakumbuka siku moja nikiwa nyumbani napiga stori na mdogo wangu sijui aliwaza nini akaniuliza swali
"hivi kaka udongo unatokana na nini?"
Nilimjibibu "udongo unatokana na kuvunjika kwa miamba na kuwa vipande vidogo sana ambavyo
tunaviita udongo"
"Kwahiyo kaka unataka kuniambia miamba inapungua ukubwaaa kilasiku"
"Ndio"
"Kwahiyo kaka milima nayo kilasiku inapungua urefu?"
Sikumbuki nilimjibu nini . ila kutokana na swali lake nimekua nikijiuliza hivi udongo unatokana na nini? nikweli unatokana na kuvunjika kwa kwa miamba
Pengine unaweza kujibu upepo, mvua na barafu zilisababisha miamba kuvunjika na kubadilika kuwa udongo,
lakini hivi karibuni Watafiti wamenijibu swali langu lakini wameniacha na mshangao nimeamua nikushirikishe na wewe
watafiti hao wanasema waligunduwa kuwa mimea ya kale kwenye nchi kavu huenda ndio chanzo muhimu ya udongo na mchanga duniani.
Miamba aina ya shale na slate ambayo iliundwa na chembe ndogondogo za udongo na mchanga inaonekana katika sehemu nyingi duniani, lakini ni nadra kugunduliwa kwenye tabaka la dunia lenye historia zaidi ya miaka milioni 500. Kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Cambridge kimechambua mabadiliko ya kiasi cha udongo uliolimbikizwa chini ya mito ya miaka bilioni 3.5 hadi milioni 300 iliyopita, na kugundua kuwa kutokana na kustawi kwa mimea ya kale kwenye nchi kavu, kiasi cha udongo kwenye nchi kavu kiliongezeka kwa kasi kubwa.
Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka milioni 458 iliyopita, udongo ulichukua asilimia 1 tu ya vitu vilivyolimbikizwa chini ya mito, kiasi hiki kiliendelea kuongezeka katika miaka milioni 100 ifuatayo, na katika kipindi kati ya miaka milioni 359 hadi miaka milioni 299 iliyopita, kiasi cha udongo kilifikia asilimia 26. Watafiti wamesema kustawi kwa kuvumwani katika miaka milioni 500 iliyopita na kuzaliwa na kuenea kwa mimea ya ngazi ya juu yenye mizizi mirefu katika miaka milioni 430 iliyopita kumesababisha kiasi cha udongo duniani kuongezeka. Lakini watu bado hawajui jinsi mimea ilivyoharakisha kutokea kwa udongo, na walikisia kuwa kemikali inayotolewa na mimea huenda ni sababu moja
je unazani nikweli udongo unatokana na mimea ya kale?
Maoni
Chapisha Maoni