FAIDA ZA KAHAWA KIAFYA
FAIDA ZA KAHAWA
Kahawa ni kinywaji kinachopendwa na watu wengi wa jamii zote duniani kama kiamsho kwa asubuhi.
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KAHAWA
1. Kahawa inaweza kukuongezea nguvu mwilini.
Kikombe cha Kahawa kinaweza kukufanya usijisikie mchovu na kukuongezea nguvu mwilini.
Hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuna kichangamsho (stimulant) kiitwacho kafeina.
2. Husaidia kuchoma mafuta mwilini
Kaffeina ni moja ya viinilishe vya asili ambavyo vimethibitishwa kuwa vinasaidia kuchoma mafuta mwilini. Tafiti kadhaa zinaonyesha kaffeina inaweza kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng;enyo wa chakula kwa asilimia 3 mpaka 11.
3. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwenye Kahawa.
Kahawa nii zaidi ya yale maji meusi. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwa mwili wa binadamu. Viinilishe hivyo ni pamoja na vitamini B5, manganizi, potasiamu, magnesiamu nk
4. Kaffeina inaweza kuwa mlinzi kwa Ini Watu wanaokunywa kahawa wana asilimia mpaka 80 za kutokupata magonjwa mbalimbali ya ini.
5. Kaffeina inaweza kukuondolea msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo au mfadhaiko ni ugonjwa hatari ambao unaweza kukupunguzia ubora wa maisha yako. Ni hali ya kawaida kwa miaka ya sasa huku ikiathiri karibu watu wengi.
Maoni
Chapisha Maoni