Jinsi ya kuwa gentlemen wa kisasa

1. Muungwana wa sasa usali na kuamini MUNGU yupo.

Kama sote tujuavyo MUNGU ndio kila kitu kwenye maisha yetu ya kila siku kwani tunapewa pumzi bure na pia anatulinda na maadui tunaowafaham na tusiowafahamu.hivo muungwana wa kisasa umuamini MUNGU na uwe na hofu ya MUNGU.





2. Vaa vizuri bila kujali tukio.

kama wengi tunavyojua kua uvaaji wako ndo unaonesha wewe ni mtu wa aina gani,hivo vaa vizuri nguo zinazokufiti mwili na zisiwe kubwa au zinazobana kupita kiasi.usivae milegezo.





3. Kutanisha macho kwa macho wakati wa kuzungumza na mtu.

Inaonyesha kiwango cha ujasiri, uaminifu na maslahi ya kweli pia uongeza mkazo kwenye kile unachokiongea.





4. Ustaarabu hauna gharama yoyote, lakini ndio kila kitu.

Kama neno linavokwenda, tabia nzuri ni hitaji daima katika mtindo, na kila muungwana wa kisasa anapaswa kujua kwamba tabia zinaweza kufungua milango ambayo elimu haiwezi.





5. Lugha mbaya inaonyesha ukosefu wa elimu.

Wakati wa kuzungumza angalia sana maneno unayotamka yasiwe yenye kuonesha dharau,matusi au kujikweza au yasinkoseshe mtu raha na amani wakati wowote ule.





6. Kuwa na taarifa nzuri juu ya matukio ya sasa.

Muungwana wa kisasa awe na taarifa nzuri juu ya matukio ya sasa aidha kwa kusoma magazeri,kusikiliza redio,mtandao na kuangalia habari tofaut tofauti katika runinga.





7. Muungwana wa kisasa sio mnafki na mmbea.

muungwana wa kisasa hawezi kumcheka mtu au kueneza uvumi usio wa kweli kwa sababu anajua yote itafanya ni kuharibu sifa yake mwenyewe.



8. Kuwa wa heshima sio ishara ya udhaifu.

Hakuna chochote dhaifu juu ya kufungua milango,kupisha kiti kwa mtu aliemzidi umri,au mjamzito au mlemavu.pia kumheshimu kila mtu wa rika yoyote. muungwana wa kisasa hauhitaji kufikiria mara mbili kuhusu hilo.





9. Tunza muonekano wako.

muungwana wa kisasa huwa na muonekano wa kuvutia.usafi,kuweka nywele katika mpangilio mzur aidha kwa kuzichana au kwa kunyoa ili mradi ziwe na muonekano msafi,kuweka ndevu pia katika muonekano wa usafi.

10. Pendezesha nyuso yako kwa tabasamu.

Muungwana wa kisasa sura yake huwa inapendezeshwa na tabasamu hata kama moyoni mwake kuna mambo magumu.wazungu wanasema "Happiness starts with a smile." tafsir " furaha uanza kwa tabasamu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

HAYA NDIO MAKUNDI 16 YA WATU NA TABIA ZAO

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA