Faida za Tangawizi, kiafya na Tiba.

Mtangawizi jina la kisayansi  Zingiber officinale ni mmea wa familia Zingiberaceae katika ngeli ya Monokotiledoni.
 Mti wa mtangawizi

Mizizi yake yanayoitwa tangawizi hutumika kama kiungo katika chakula na unga wake hutumika katika vinywaji na katika chakula pia.
Mzizi wa Mtangawizi


FAIDA 48 ZA  TANGAWIZI
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni
6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
7. Huondoa maumivu ya koo
8. Huua virusi wa homa
9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini
10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)
14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)
16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo
17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi
19. Huongeza msukumo wa damu
20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo
21. Huzuia damu kuganda
22. Hushusha kolesto
23. Husafisha damu
24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
25. Hutibu shinikizo la juu la damu
26. Husafisha utumbo mpana
27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha
35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
41. Huimarisha afya ya figo
42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha
44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

UNYWAJI WA TANGAWIZI- FAIDA KUMI UTAKAZOZIPATA UKIANZA KUNYWA LEO.
Pamoja ya kwamba Tangawizi ina faida nyingi ifuatayo Ni faida ya Tangawizi endapo utainjwa

1.Huondoa Harufu mbaya ya kinywa.
Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo yamdomo kuwa safi
2.Msukumo Wa Damu
Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwilini kwasababu huupa mwili joto ambalo mara nyingi mwili huhitaji wakati wa usukumwaji wa damu mwilini.
3.Huondoa Magonjwa ya Asubuhi
Licha ya kuwa tiba ya magonjwa kama Kikohozi na Mafua, Tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu, na mning’inio. Kwa akina mama wajawazito, Tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka, pia hutumika kama kichocheo cha utulivu.
4.Mfumo wa Chakula
Husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula. Hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu.
5.Kurekebisha Sukari ya Mwili
Tangawizi husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu. Wagonjwa wa Kisukari wanashauriwa kutumia Tangawizi badala ya chai.
6.Hamu Ya Kula (appetizer)
Huongeza hamu ya kula chakula. Kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.
7.Uzalishaji wa MateTangawizi
Unywaji wa Tangawizi husaidia uzalishaji wa mate mdomoni. Kuongezeka kwa mate mdomoni husaidia kutengeneza vichocheo Muhimu vinavyosaidia wakati wa kula, na hupunguza pia uwezekano wa magonjwa ya meno.
8.Kuyeyusha Mafuta
Tangawizi husaidia kupunguza Kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini. Hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu.
9.Kuondoa Sumu Mwilini
Tangawizi husaidia kupunguza kichefuchefu na kutapika. Pia huwasadia sana wale watu waliotumia sana madawa na kuwa na  sumu nyingi mwilini.
10.Tangawizi Pia humsaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda hivyo kama vitakuwa kwenye hatua ya awali sana!.

Tangawizi na Nguvu za kiume
Chai ya Tangawizi

Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Hivyo hufanya umee(mboo) kuwa imara
Hinaweza ikiwa Tangawizi italiwa ikiwa  mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. 
Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Na kuweka sukari ili uweze kuinjwa, vilevile badala ya kutumia sukari wewe  unaweza ukatumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

HAYA NDIO MAKUNDI 16 YA WATU NA TABIA ZAO

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA