Ujumbe mkongwe zaidi uliohifadhiwa kwenye chupa
Familia moja nchini Australia umepata ujumbe ambao ni mkongwe zaidi uliokuwa umehifadhiwa katika chupa,
Ni takribani miaka 132 tangu ujumbe uliokuepo kwenye chupa urushwe katika bahari.
Chupa hiyo yenye ujumbe iliokotwa na bwana Tonya Illman wakati akiwa anafanya matembezi katika ufukwe wa bahari huko pembezoni,magharibi mwa Australia.
Wakati ameokota chupa hiyo ,Tonya hakujua ni nini kilichoandikwa mpaka alipofika nyumbani kwake na kuioka karatasi hiyo katika jiko la kuokea(Oven).
Wataalamu wamethibitisha kuwa ujumbe huo ni wakweli na ulitupwa kutoka meli moja ya Ujerumani.
Ujumbe huo uliokuwa umeandikwa tarehe 12.6.1886, na ilikuwa sehemu ya jaribio ambalo lilifanywa na meli hiyo ya ujerumani ili kubaini njia ambayo meli za taifa hilo zilikuwa zinapita baharini.
Miaka iliyopita kumbukumbu za "Guiness world "zilisema ujumbe ambao uliowahi kutupwa kwa kuhifadhiwa kwenye chupa na kupatikana ulikaa miaka 108.
Hata hivyo mtu huyo alipoliokota ujumbe huo alidhani labda hiyo sio tarehe sahihi ambayo iliandikwa kwa kuwa ilikuwa imefifia sana hivyo ukadhania pia labda ni kweli hivyo aliaua kuupeleka kwa wataalamu makumbusho nchini humo.
Na cha kushangaza walikuta muandiko huo unafanana na jarida ambalo lilitengenezwa na nahodha tarehe hiyo hiyo na mwandiko ukiwa unafanana
Chanzo bbc
Maoni
Chapisha Maoni