AFYA:KUCHEZA DANSI KUNAPUNGUZA KUZEEKA KWA UBONGO

Utafiti mpya umeonesha kuwa ikilinganishwa na mazoezi rahisi ikiwemo kutembea, kucheza dansi kunaweza kupunguza zaidi uzeekaji wa ubongo.

Utafiti wa awali umeonesha kuwa mazoezi yanaweza kuusaidia ubongo kupambana na uzeekaji, lakini haukuonesha mazoezi ya aina gani ni mazuri zaidi. Utafiti huo mpya umelinganisha mazoezi ya aina mbili tofauti yaani kucheza dansi na mazoezi ya uvumilivu. Matokeo yameonesha kuwa kucheza dansi ni nzuri zaidi.

Watafiti wa Ujerumani wamewashirikisha wazee waliojitolea wenye umri wa wastani wa miaka 68. Katika utafiti wa miezi 18, wazee hao wote wamejifunza kucheza dansi au kufanya mazoezi ya uvumilivu kila wiki.

Kikundi cha mazoezi ya uvumilivu kinatakiwa kurudia kufanya mazoezi ambayo ni pamoja na kupanda baiskeli na kutembea. Kikundi cha kucheza dansi kinatakiwa kujifunza mtindo mpya wa dansi kila wiki.

Kutokana na uangalizi wa eneo la Hippocampus la ubongo, mazoezi hayo mawili yote yanaweza kuinua uwezo wa eneo hilo, lakini kucheza dansi kunaweza kuinua dhahiri uwezo wa uwiano wa wazee, hivyo kucheza dansi kunatoa mchango katika mapambano dhidi ya uzeekaji wa ubongo.

Eneo la hippocampus ni eneo linalohusiana na uwezo wa kumbukumbu, ufahamu na uwiano. Katika mchakato wa uzeekaji, udhoofishaji wa uwezo wa eneo la hippocampus unaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa ufahamu na uwezo wa mazoezi

Tuandikie maoni yako

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

HAYA NDIO MAKUNDI 16 YA WATU NA TABIA ZAO

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA