Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya jifunzenami

SABABU NANE ZINAZOSABABISHA WATU KUWA NA TABIA YA HASIRA AU KITABIA

SABABU NANE ZINAZOSABABISHA WATU KUWA NA TABIA YA HASIRA AU KUSHINDWA JIDHIBITI KITABIA Hasira ni hisia, kila mwanadamu anazaliwa nayo ila tuna viwango tofauti kutokana na kila mmoja wetu kimaumbile anavyoweza kukabiliana na mazingira yenye vichocheo vya tabia hiyo ya hasira na kujidhibiti  mwanadamu wana  vichocheo vinaweza  kuhisi umedharauliwa, kutotendewa haki, kuvunjiwa heshima au kupuuzwa. Hivi ndiyo vichocheo vikubwa vya tabia hiyo lakini zipo sababu nyingine nyuma ya pazia wengi tusizo zijua. Ambazo nyingine hukaa katika ufahamu wa ndani (Unconscious) na zimekuwa zikiendesha tabia zetu au zikichangia tabia hii na kutufanya haraka hasira kwenda kwenye ghadhabu ni jambo dogo sana.     1.Maumbile ya Ubongo na tabia za kurithi Maumbile ya ubongo wa binadamu mfano kunapokuwa na shida au hitilafu hasa mishipa inayounganisha sehemu za ubongo. Yaani eneo la ubongo linaloitwa “Amygdale” linalohusika na hisia ikiwemo hasira...

FAIDA ZA KAHAWA KIAFYA

Picha
FAIDA ZA KAHAWA Kahawa ni kinywaji kinachopendwa na watu wengi wa jamii zote duniani kama kiamsho kwa asubuhi. ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KAHAWA 1. Kahawa inaweza kukuongezea nguvu mwilini. Kikombe cha Kahawa kinaweza kukufanya usijisikie mchovu na kukuongezea nguvu mwilini. Hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuna kichangamsho (stimulant) kiitwacho kafeina. 2. Husaidia kuchoma mafuta mwilini Kaffeina ni moja ya viinilishe vya asili ambavyo vimethibitishwa kuwa vinasaidia kuchoma mafuta mwilini. Tafiti kadhaa zinaonyesha kaffeina inaweza kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng;enyo wa chakula kwa asilimia 3 mpaka 11. 3. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwenye Kahawa. Kahawa nii zaidi ya yale maji meusi. Kuna viinilishe kadhaa vizuri kwa mwili wa binadamu. Viinilishe hivyo ni pamoja na vitamini B5, manganizi, potasiamu, magnesiamu nk 4. Kaffeina inaweza kuwa mlinzi kwa Ini Watu wanaokunywa kahawa wana asilimia mpaka 80 za kutokupata magonjwa mbalimbali ya ini. 5. Kaffeina inaweza kukuondolea m...

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

Picha
ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO Msongo wa mawazo unajulikana kama sehemu ya maisha ya kawaida. Mwili wako unaweza kuitikia hali hii kiakili na kimwili. Hata hivyo msongo wa mawazo unaweza kusababisha athari mbaya kwako.zifuatazo ni athari mbaya za msongo wa mawazo.(8) 1. Uharibu mzunguko wa usingizi kwanza ya madhara ya juu ya msongo wa mawazo kwenye mwili ni kuvuruga mzunguko wako wa usingizi. Inaweza kuathiri vibaya juu ya ubora wa usingizi wako na kusababisha kukosekana kabisa kwa usingizi. Kama tunavojua usingizi ni sehemu muhimu ili kuhakikisha afya yako kuwa nzuri na usingizi huweza kusababisha madhara hasi kwa afya yako ya akili na ya kimwili kama ukikosekana.ukiona umekosa kabisa usingizi kwa sababu ya msongo wa mawazo inapaswa umuone daktari. 2. Huvuruga mfumo wako wa chakula mwilini. Moja ya athari mbaya ya msongo wa mawazo kwenye mwili ni kuvuruga mfumo wa chakula. Kuvuruga homoni, kupumua haraka, na moyo kwenda kasi ni mambo makuu matatu ambayo huvurug...

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA

Picha
JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA karibu tena kwenye jiko na mapishi na tunajifunza kupiki lost ya nyama. Viongo vyanavoitajika ➡Nyama 1kg ➡Nyanya 2 kubwa zioshwe kisha zikatwekatwe ➡Pilipili hoho 1 kubwa ➡karoti 1 kubwa hakikisha ni safi ➡Thomu iliyo sagwa 1 kijiko cha chai ➡Tangawizi iliyo sagwa 1 kijiko cha chai ➡Chumvi kiasi ➡Kitunguu maji 1kikubwa ➡Royco packiti moja JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA 1. chukua nyama yako ikatekate vipande unavyo itaji,na uioshe iwe safi. 2.Chukua tangawizi yako ioshe na isage kisha iweke tangawizi ambayo umesha isaga changanya na iweke chumvi kiasi na uibandike jikoni ,usubili mpaka iive vizuri ,na uiipue ikiwa imeiva. 3. Bandika sufuria na uweke mafuta kiasi,na yakipata moto weka vitunguu vyako vikaange mpaka vibadilike rangi na uweke hoho na karoti navyo vichanganye 4. kisha chukua nyanya nazo zitie kwenye ule mchanganyiko woko, koroga nyanya baada ya muda kidogo weka t...

COBRA: NYOKA HATARI MWENYE SUMU KALI

Picha
COBRA: NYOKA HATARI MWENYE SUMU KALI NYOKA ameorodheshwa katika kundi la viumbe 10 hatari kwa maisha ya binadamu kutokana na kuwa na sumu kali inayoweza kuua katika muda mfupi, au kuleta madhara makubwa. Hata hivyo, si nyoka wote walio hatari kwa binadamu isipokuwa baadhi yao tu akiwemo nyoka aina ya Cobra, ambaye anapatikana sehemu nyingi duniani, lakini zaidi katika ukanda wa Bahari ya Hindi, Pacific na Jangwa la Sahara. Cobra ana tabia ya kupenda kujificha, na mara nyingi huwa hapendi kuonekana kwenye maeneo wanayoishi zaidi watu. Watafiti wanasema kuwa, tabia zake za kutopenda kuonana na watu au kuishi kwenye mazingira kama hayo, ni kutokana na kutambua kwamba binadamu ni adui yake mkubwa. Kimaumbile Cobra wako wa aina nyingi hali inayowafanya kutofautiana kimaumbo, tabia, mazingira ya kuishi na umri pia. Hata hivyo, Cobra mrefu zaidi anaweza kufika urefu wa futi sita au zaidi. Ana uwezo wa kutambaa kwa kasi iwe kwenye mchanga au majani, kusimamisha kichwa juu na kurusha mat...

FAIDA ZA MMEA WA MCHAICHAI

Picha
FAIDA ZA MMEA WA MCHAICHAI Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai. Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya. 1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani . Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani. 2. Hutibu magonjwa ya kuhara . Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi. Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa meng...

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo Wajasiriamali waliofanikiwa wanafahamu na wanaziishi sifa za wajasiriamali bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa mjasiriamali bora wakati una sifa za mwajiriwa. Ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuzifahamu na kuziishi sifa za mjasiriamali. Karibu nikufahamishe sifa 10 za mjasiriamali. 1. Mwenye malengo Malengo ni mwongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Je umeamua kuwa mjasiriamali kwenye nini? Kwa ajili ya nini? Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila mwongozo wowote na ni vigumu kufanikiwa. Siku zote huwezi kujiita masafiri hujui unaenda wapi utakua hunatofauti na MTU aliyepotea njia Ili uwezi kufanikiwa lazima uwe na malengo  yawe kama ndio mmongozo wako 2. Nidhamu Nidhamu ni sifa muhimu kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali...

UNAYAKUMBUKA HAYA: UFO,ALIENS VIUMBE WA AJABU

Picha
UFO,ALIENS VIUMBE WA AJABU UFOs ni Vyombo vyenye ukubwa tofauti na maumbile tofauti ambapo vingine vinakadiliwa kuwa na ukubwa wa futi 100 ama zaidi vingine na muonekano wake ni wa duara kama sahani kubwa la chuma lenye kung'a(steel shaped-saucer), lakini pia vinaweza kuwa na umbo mengine tofauti kama vile maumbile ya pembe tatu ambapo kwa chini zinakuwa ya na taa zenye kutoa miale mikali ya mwanga yenye rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe. UFOs ndizo zinabeba viumbe wajulikanao kama Aliens na viumbe hawa wanamaumbo kama ya binadamu lakini tofauti yake iko katika macho na vidole kwani viumbe hawa wana macho makubwa yenye umbo la ovali, vidole vikubwa vitatu badala na wakati mwingine mikono mirefu, na miili yao ni kama yenye hali ya mpira hivi na wakati mwingine waonekanapo wanakuwa kama waliovalia aina ya kama nguo zenye kubana mwili mzima zenye rangi ya bluu na mikanda viunoni mwao, hakika viumbe hivi vinatisha kimuonekano wao. Taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo mba...

vichekesho na vimbwanga vya mitandaoni

*Madem mna roho MBAYA kweli* *Unakutana na dem mgahawani* *Una mpa ofa ya* *supu ya mbuzi* *Baadae una mpa* *hela ya taxi* *Cha ajabu ukimpa namba ya simu* *Anakusave* *SUPU YA MBUZI* 😢😢😢 *HIVI KWANINI* ............................................................ 🤔🤔 *Wakati mzungu katengeneza simu, na unaitumia kwa mawasiliano ya video(video call/snap video) kisha unaita teknolojia...🙆‍♂🙆‍♂Chakushangaza bibi yako akitumia kioo kukuangalia unapokua mbali eti waita uchawi...🤣😂🤣😂🤣😂hivi waafrika tuna laana gani??🙆‍♂🙆‍♂🙆‍♂* ............................................................ *Wife :Baby leo nimeona iphone8 kwenye duka la simu mjini, ni nzuri😍 *Husband : Vipi umeipenda🤔 *Wife: Nimeipenda sana mpenzi wangu😍😍😜&#128540...

jinsi ya kumiliki biashara yako

Watu wengi wamekua wamitamani kumiliki biashara au kuwa wajasiriamali lakini hawajui ni njia gani wafuate  leo nimekuandalia haya kwa uchache ufikie ndoto zako Usiruhusu orodha hii kukuogopesha. Hatua ya kwanza ya kuwa na mafanikio ni kuelewa ujuzi gani unao na ambao unakosa. Stadi hizi zote unaweza kujifunza, kwa hivyo ukitambua unakosa kitu fulani,usisite kujifunza. Linapokuja suala la mauzo, masoko na fedha unaweza kuchukua kozi, kujifunza mwenyewe au kujifunza kutoka kwa watu walio karibu nawe. ukishafahamu utakuwa tayari kuzindua biashara yako. 1. Uwezo wa kusimamia fedha Ili kuendesha biashara kwa ufanisi. unahitaji kuwa na uwezo wa kusimamia fedha. Jibu maswali haya kuhusu fedha zako binafsi kwanza: Unajua wapi fedha zako huenda kila mwezi? Je, unazalisha zaidi ya unayotumia? Ikiwa jibu sio kwa yote mawili, utajitahidi kusimamia pesa yako na biashara pia. Anza kwa kupata fedha zako binafsi, utumie kwa utaratibu kwa kuzingatia bajeti ya biashara. 2. Uwezo wa kuzalisha. H...

SAYANSI: Wanasayansi wamevumbua betri ya li-on inayowezakutumika kwenye joto la

Picha
     Wanasayansi wa China wamesanifu betri ya Li-ion inayoweza kutumiwa katika joto la nyuzi 70 sentigredi chini ya sifuri, ambayo inatazamiwa kutumiwa katika maeneo yenye baridi kali duniani na hata anga ya juu.      Kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Fudan kinachoongozwa na Xia Yongyao kimetumia kemikali aina ya Ethyl Acetate inayoweza kupitisha umeme katika mazingira yenye baridi kali kuwa elektrolaiti, na kutumia kemikali za kikaboni za PTPAn na PNTCDA kuwa elektrodi mbili.       Elektrolaiti ni kemikali inayozifanya ioni zitiririke kati ya elektrodi mbili za betri, lakini mabadiliko ya kikemikali kati ya elektrolaiti na elektrodi hayawezi kudumu katika mazingira yenye baridi kali.       Uwezo wa betri ya zamani ya Li-ion katika joto la nyuzi 20 sentigredi chini ya sifuri unapungua na kuwa nusu tu, na uwezo huo umepungua hadi kuwa asilimia 12 tu ya hali ya kawaida katika joto la nyuzi 4...

AFYA:KUCHEZA DANSI KUNAPUNGUZA KUZEEKA KWA UBONGO

Utafiti mpya umeonesha kuwa ikilinganishwa na mazoezi rahisi ikiwemo kutembea, kucheza dansi kunaweza kupunguza zaidi uzeekaji wa ubongo. Utafiti wa awali umeonesha kuwa mazoezi yanaweza kuusaidia ubongo kupambana na uzeekaji, lakini haukuonesha mazoezi ya aina gani ni mazuri zaidi. Utafiti huo mpya umelinganisha mazoezi ya aina mbili tofauti yaani kucheza dansi na mazoezi ya uvumilivu. Matokeo yameonesha kuwa kucheza dansi ni nzuri zaidi. Watafiti wa Ujerumani wamewashirikisha wazee waliojitolea wenye umri wa wastani wa miaka 68. Katika utafiti wa miezi 18, wazee hao wote wamejifunza kucheza dansi au kufanya mazoezi ya uvumilivu kila wiki. Kikundi cha mazoezi ya uvumilivu kinatakiwa kurudia kufanya mazoezi ambayo ni pamoja na kupanda baiskeli na kutembea. Kikundi cha kucheza dansi kinatakiwa kujifunza mtindo mpya wa dansi kila wiki. Kutokana na uangalizi wa eneo la Hippocampus la ubongo, mazoezi hayo mawili yote yanaweza kuinua uwezo wa eneo hilo, lakini kucheza dansi kunaweza kui...