Jinsi ya kuchagua perfume zuri

Kuna maelfu ya perfume madukani, lakini sio perfume zote ni nzuri kwa kila mtu, kwa hiyo ni muhimu kuchagua perfume ambayo itamfaa mtumiaji ili kuepuka disappointment.

Perfume unapoinusa inagawanyika mara tatu, wenyewe wanaita NOTES, yani kile unachokisikia na ukali wake unavotofautiana. Hiyo ndo sababu perfume zingine ukinunua ukajipuliza zinakuwa kama harufu inabadilika kadri inavosikika inapojichanganya na hewa, zingine hupoteza mvuto kabisa wakati nyingine huendelea kupendeza kadri mda unavoenda. 

Hizi notes ziko tatu, Top Note(Harufu unayoisikia mwanzo kabisa) ambayo inapotea haraka, kuna middle note yaani harufu ya kati ambayo utaisikia baada ya harufu ya mwanzo kupotea na mwisho Note ya tatu ambayo huitwa Basic Note yani harufu haswa ya hiyo perfume baada ya harufu za mwanzoni kupita,ambayo ndo itabaki muda mrefu. Inashauriwa unapochagua perfume ya kununua usilipe mpaka umeisikia vizuri mpk mwishoni hata dakika 20 hivi.

Perfumes hugawanywa kulingana na aina ya harufu ambazo kwa upande mwingine zinaamua ipi ni ya kiume na ipi ya kike. Aina za harufu hutofautiana kutokana na viungo vilivyotumika kutengeneza. Mgawanyiko huu ni citrus, fresh, floral, oriental, sweet, spice, or wood kwa perfume za wanawake. Na kwa perfume za wanaume viungo ni leather, tobacco, musk, na mosses.

Perfume zimegawanyika kwa aina (au madaraja)

Eau de Cologne

Hii mara nyingi ina harufu laini na inatokana na mchanganyiko wa asilimia 3-5% ya mafuta ya perfume yenyewe ikiwa imechanganywa na maji na alcohol. Mara nyingi harufu yake hutokana na mafuta ya matunda jamii ya limao/chungwa (citrus fruits).

Eau de Toillete

Hii ina kiungo cha mafuta ya perfume kwa asilimia sawa na cologne au huweza kuzidi kidogo, kuanzia asilimia 4-8% ikiwa imechanganywa na alcohol pekee bila maji.

Eau de Parfum

Hii ina gharama ukilinganisha na na cologne au de toillete kwa sababu mafuta ya perfume huwekwa zaidi kufika 15-18% yakiwa yamechanganywa na alcohol.

Perfume

Ukiona kitu kinaitwa Perfume sasa basi humo ndani percentage ya mafuta ya perfume ni kubwa ukilinganisha na hayo majina mengine, humu hufikia asilimia 15-30%. Pia hii ni gharama zaidi.

Jinsi ya Kuchagua inayokufaa

1. Usifanye haraka kununua perfume, chukua muda kutafuta perfume nzuri.

1. Chagua harufu unayojisikia vizuri ukiisikia

Ni vema uchague perfume inayokupa hisia nzuri, inayokufanya ujipende na ujisikie vizuri.

2. Zingatia jinsi ulivyo

Hapa ni vema ukajijua wewe ni mtu wa aina gani na unapenda kuonekana vipi. Kama wewe ni mtu mkimya unaetaka utulivu sana basi chagua harufu nyepesi au laini mfano harufu za vanilla nk. Na iwapo wewe ni mtu unayependa kuonekana na kugeuza shingo za watu unapopita basi pia chagua perfume itakayokutambulisha kuwa unapita au umepita hapo.

3. Jaribu kuisikiliza perfume kwanza kabla hujanunua
Hii itakuhakikishia kwamba unanunua kitu unachokitaka. Kama hujaisikiliza/nusa vema inaweza kuwa moja ya zile perfume zinazobadilika harufu mwishoni hivyo kuwa kwazo kwako na wengine watakaoipata harufu ya perfume yako.

4. Shirikisha mtu mwingine katika kuchagua harufu nzuri
Hii itasaidia kuchagua perfume nzuri ambayo haitakwaza watu watakaokuzunguka aidha kiafya (alergy ya harufu kali) au kihisia.

5. Usinunue perfume kwa kuchagua jina la perfume au brand name au muonekano tu no! kama hauijui kwani majina mengine ni matangazo tu na hai-reflect juice iliyopo ndani na inaweza isiendane na vigezo hapo no.2 ambavyo ni muhimu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO

HAYA NDIO MAKUNDI 16 YA WATU NA TABIA ZAO

JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA