SABABU NANE ZINAZOSABABISHA WATU KUWA NA TABIA YA HASIRA AU KITABIA
SABABU NANE ZINAZOSABABISHA WATU KUWA NA TABIA YA HASIRA AU KUSHINDWA JIDHIBITI KITABIA
Hasira ni hisia, kila mwanadamu anazaliwa nayo ila tuna viwango tofauti kutokana na kila mmoja wetu kimaumbile anavyoweza kukabiliana na mazingira yenye vichocheo vya tabia hiyo ya hasira na kujidhibiti mwanadamu wana vichocheo vinaweza kuhisi umedharauliwa, kutotendewa haki, kuvunjiwa heshima au kupuuzwa. Hivi ndiyo vichocheo vikubwa vya tabia hiyo lakini zipo sababu nyingine nyuma ya pazia wengi tusizo zijua.
Ambazo nyingine hukaa katika ufahamu wa ndani (Unconscious) na zimekuwa zikiendesha tabia zetu au zikichangia tabia hii na kutufanya haraka hasira kwenda kwenye ghadhabu ni jambo dogo sana.
1.Maumbile ya Ubongo na tabia za kurithi
Maumbile ya ubongo wa binadamu mfano kunapokuwa na shida au hitilafu hasa mishipa inayounganisha sehemu za ubongo. Yaani eneo la ubongo linaloitwa “Amygdale” linalohusika na hisia ikiwemo hasira. Na sehemu ya ubongo wa mbele yaani katika paji la uso (Front Brain). Eneo hili huwa linahusika sana na fikra za uamuzi na utambuzi, nini cha kufanya katika mazingira unakutana nayo kila leo.
Hivyo kunapotokea shida katika mishipa hiyo inayounganisha “Amygdala” na “frontal brain”Mtu mwenye tatizo hilo huwa hasira yake ni mpaka haitimize kile alichokusudia.
Vile vile sababu nyingine ni kurithi tabia kutoka katika familia, ukoo na hata kabila. Yapo makabila ambayo hasira ina nafasi yake, na mara utakuta mtu akijisifia au wapo wanaojionea ufahari tabia ya Hasira
Labda tunafahamu baadhi ya mikoa ambayo ina udhaifu wa tabia hiyo na mara nyingi kumekuwa na habari za matukio ya kufanyiana ukatili wa kutisha au wengine kujiua pale wanapoudhiwa na kuwa hasira.
2. Magonjwa ya akili na kuadhirika kisaikolojia
Yapo magonjwa ya kisaikolojia ambayo yanatokana na mabadiliko ya kupungua au kuzidi kwa kemikali za mwilini hasa kwenye ubongo hivyo inapelekea mabadiliko ya kihisia pasipo mpangilio mfano wa magonjwa hayo ni Bipolar Disorder ambapo humfanya mtu kuwa na hisia au mabadiliko yasiyo ya kawaida ya kihisia.Na usababishwa na shida za kemikali katika ubongo Serotonin, dopamine , na
norepinephrine
3. Nadharia ya Kujifunza tabia,
Kwa tabia za kujifunza hupo msemo unaosema “mbuyu ulianza kama mchicha” na “samaki mkunje angali mbichi”. Hisia za hasira sababu huwa ndani ya binadamu huwa zinasubilia kichochezi na huwa zinafikia kukomaa na moja ya vichochezi hivyo ni aina ya miziki inayohamasisha vurugu, Michezo ya kompyuta na televisheni yaani nikimaanisha “Video Games” na vipindi vyenye kuchochea vurugu na mauaji au vita. Kama unataka kupona tabia hiyo anza kuepuka vichochezi kama hivi visivyo vya lazima sana kwani “safari ya maili elfu moja ilianza na hatua moja”
4. Marafiki tunaokuwa nao,
Katika eneo la marafiki kuna sheria moja katika saikolojia inaitwa Law of Proximity yaani vitu vinaavyoambatana pamoja ni vimoja na katika Kiswahili pia kuna msemo
huo “Ndege wanaofanana huruka pamoja” tabia ni kama ugonjwa huwa zinaambukizana hasa kwa marafiki na watu wa karibu ambao ni negative au hasi.
5. Mapito au matukio wakati wa miaka ya utotoni
Unapopitia maisha ya watu wengi ambao walifanya mambo ya kushtua ulimwengu kutokana na kuwa ya kutisha na kuoghofya au ya kikatili.
Rudi nyuma ukaangalie sehemu za maisha waliopitia si tu hao wapo wengine walibakwa au kunajisiwa. Au waliteswa na walezi wao au wazazi wao hivyo maisha hayo yamewaachia alama ndani ya mioyo yao. Na wengine imewazalishia tabia ya hasira iliyokomaa yaani ghadhabu. “Tofauti ya mtoto mvulana na Mwanaume ni aina ya mdoli wa gari wanaouchezea”
6. Mazingira, mazingira huchochilea mabadiliko ya kitabia mfano,
Kushuhudia mzazi wako mmoja akipigwa au akinyanyaswa au kutelekezwa na ndugu jamaa na na masuala yanayohusu wazazi kutalikiana, na zipo sababu nyingine za kijamii mfano mapigano ya labda ya wakulima na wafugaji, au kushuhudia vita au namna ya ubaguzi.
7.Mabadiliko yanayogusa homoni
Mabadiliko hasa wakati wa kubarehe yaani kutoka katika utoto kwenda katika ujana “Adolescence”. Wakati huu kuna vijana hujikuta kuwa na hasira za karibu ambazo huzitoa kwa namna ya kiburi
Pia mabadiliko hasa kihomoni vile hata mwanamke anapokuwa katika kipindi cha ujauzito pia yanachangia tabia ya hasira na maranyingi hushindwa kujizibiti hasira zao
8. Matumizi ya vilevi
Yapo matumizi ya vilevi Kama vile Bangi, heroine na Cocaine ambayo husabaisha mabadiliko ya kemikali katika Ubongo wa binadamu hivyo yanapelekea mtu kutokuwa sawa kihisia.
Na kuwa na hasira za ajabu kwa sababu hushindwa kujidhibi na hasira
Unapokuwa na mlevi ni rahisi kugombana naye
Imeandaliwa na : Gift Mshana
Simu. : 0712400898
Email : giftmshana0712@gmail.com
Usikose makala nyingine hapa
Maoni
Chapisha Maoni